• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa NATO na Russia waanza tena

    (GMT+08:00) 2016-04-21 19:14:32

    Baraza kati ya Jumuiya ya NATO na Russia limeitisha mkutano wa mabalozi huko Brussels kujadli ajenda ya masuala ya Ukraine na Afghanistan, na udhibiti wa hatari. Huu ni mkutano wa kwanza kufanywa na baraza hilo tangu utaratibu wa mkutano usitishwe miaka miwili iliyopita kutokana na mgogoro wa Ukraine. Lakini baada ya mkutano huo pande zote mbili zimesema, hazijapata maendeleo makubwa katika kupunguza mvutano unaoongezeka katika uhusiano wa kijeshi kati yao.

    Mkutano wa mabalozi wa Baraza kati ya NATO na Russia umendeshwa na katibu mkuu wa Jumuiya hiyo Bw. Jens Stoltenberg, na kuhudhuriwa na mjumbe wa kudumu wa Russia katika jumuiya hiyo Alexander Grusko. Baada ya mkutano huo, Bw. Stoltenberg amesema, hivi sasa kuna tofauti kubwa ya maoni kati ya Russia na NATO.

    (Sauti 1)

    "Jumuiya ya NATO na Russia hivi sasa bado zina tofauti kubwa ya maoni, mkutano wa leo umeshindwa kubadilisha hali hiyo. Nchi wanachama wa jumuiya hiyo zinaona kuwa, ni mpaka pale Russia itakapoheshimu tena sheria za kimataifa, ndipo ushirikiano halisi utarejeshwa."

    Mkutano huo umejadili suala la Ukraine, uwazi wa operesheni husika za kijeshi, udhibiti wa hatari na suala la Afghanistan. Akizungumzia suala la Ukraine, Bw. Stoltenberg amesisitiza tena kuwa Jumuiya ya NATO inaunga mkono msimamo wa kulinda ukamilifu wa ardhi na mamlaka ya Ukraine. Jumuiya hiyo na Russia zimekubaliana kutekeleza kikamilifu makubaliano ya Minsk haraka iwezekanavyo.

    Kwa upande wa uwazi wa operesheni za kijeshi na udhibiti wa hatari, Bw. Stoltenberg amesema, pande mbalimbali zina wajibu wa kuhakikisha hali ya kikanda inatabirika, na kulinda imani na utulivu wa kanda nzima. Jeshi la kila nchi na kila muungano wa kijeshi zina haki ya kufanya mazoezi ya kijeshi, lakini jumuiya hiyo inaona kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, uwazi wa operesheni za kijeshi umepungua.

    (Sauti 2)

    "Nchi wanachama wa Jumuiya ya NATO zinafuatilia tukio la ndege za kivita za Russia kuingilia zoezi la kijeshi lililofanywa na jeshi la Marekani na Jeshi la Poland katika bahari ya Baltic. Cha muhimu ni kufahamu hatua gani tunazoweza kuzichukua ili kuongeza uwazi na kufanya hali itabirike."

    Stoltenberg amesema kuongeza uwazi wa operesheni za kijeshi kunasaidia amani ya bara la Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako