• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukumbi wa maonesho ulioko katika kambi la wakimbizi wa Wapalestina

    (GMT+08:00) 2016-05-10 07:01:00

    Katika kambi ya wakimbizi iliyoko mjini Jenin, kaskazini mwa ukanda wa Mto Jordan, upo ukumbi maalum wa maonesho, ambao ulijengwa mwaka 2006 na mwigizaji, mwongozaji na mwanaharakati wa kijamii maarufu wa Israel Bw. Juliano Mer Khamis. Katika miaka 10 iliyopita, ukumbi huo unaoitwa "Uhuru" umehuhudia masikitiko na pia matumaini ya vijana na wasichana wa Palestina wanaoishi kwenye maeneo yanayokaliwa na Israel.

    Katika darasa moja la kufanyia mazoezi kwenye ukumbi huo, watoto wa kipalestina wenye umri wa miaka kati ya 9 hadi 14 wanaonesha mchezo wa kuigiza ambao wameuandaa na kuuongoza wao wenyewe. Mohammed Lahlouh mwenye umri wa miaka 12 aliandika hadithi ya mchezo huo mfupi.

    "Hadithi yetu inaeleza maisha ya kila siku ya watu wa Palestina, ambayo yanakumbwa na migogoro, mapambano na mauaji. Igizo uliloliona linahusu wanajeshi wa Israel kuwaelekezea bunduki wapalestina na kuwapiga, migogoro kama hii inatokea kila siku hapa kwetu, hii ni hadhiti isiyo na mwisho."

    Kuzaliwa na kukomaa katika mazingira ambayo maeneo yao yanakaliwa na migogoro ya mara kwa mara, na kuona watu wazima wenye hasira wakichukua silaha kupambana na wanajeshi wa Israel, inasababisha watoto wanaoishi katika kambi za wakimbizi kuathiriwa kisaikolojia. Msimamizi wa Ukumbi wa Uhuru ambaye pia ni kiongozi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa watoto na vijana kwenye ukumbi huo Bw. Ahmead Tobasi alisema, wanajitahidi kujaribu kuwafanya watoto waeleze mawazo yao bila kuzuiliwa kwa kupitia michezo ya kuigiza, na kuwaongoza wafahamu hatua kwa hatua kwamba kupambana na vitendo vya kimabavu kwa kutumia vitendo hivyo hivyo haiwezekani kutatua matatizo yaliyopo.

    "Unadhani tunatakiwa kufanya nini? Afadhali tuchukue bunduki kushiriki kwenye mauaji, au tufanye juhudi kama vile kusafisha barabara zetu? Tuambieni mawazo yenu halisi. Tusiwafanye waisrael kusema kuwa watoto wanaoishi katika kambi za wakimbizi wanajua tu mambo ya kimabavu, hii itawaletea visingizio vingi zaidi kutushinikiza kwa kutumia silaha. Kinyume chake, tunatakiwa kuonesha utamaduni wetu wa aina tofauti, tutaendelea kujadili mambo hayo kwa kina zaidi, na njia gani tutatumia kueleza mawazo yetu"

    Jina la awali la Ukumbi wa Uhuru lilikuwa ni Ukumbi wa Jiwe, ambao ulijengwa na mwanaharakati wa haki za binadamu wa Israel Arna Mer Khamis. Bibi huyo alitumai kufanya watoto wapalesina walioathiriwa kisaikilojia wakati wa Mapinduzi ya kwanza ya Wapalestina wapate nafuu moyoni mwao kwa kupitia kufundishwa sanaa. Lakini mwaka 2002 ukumbi huo uliharibiwa na jeshi la Israel katika "vita vya Jenin", ambapo pia baadhi ya wanafunzi wa bibi Arna waliuawa.

    Baada ya miaka kadhaa, mtoto wa Arna aitwaye Juliano Mer Khamis na mwanafunzi wake Zakaria Zubeidi waliamua mpango wa mafunzo ya sanaa ya uigizaji kwa vijana na wasichana wa Palestina wa enzi mpya. Baadaye mwanaharakati wa haki za binadamu myahudi kutoka Sweden Jonatan Stanczak alijiunga na mpango huo. Mwaka 2006, Ukumbi wa Uhuru ulizinduliwa katika kambi la wakimbizi la Jenin. Bw. Stanczak alikuwa ni muuguzi, mchango kwake katika shughuli za Ukumbi wa Uhuru kunamaanisha kuendeleza kazi yake ya uokoaji.

    "Kazi yangu kwa sasa ina maana kubwa zaidi kuliko niliyozifanya katika kitengo cha dharura. Kwani kuwafanya watu wawe na afya njema sio tu kuweka dawa kwenye vidonda, bali tunatakiwa afya ya mwili, moyo na saikolojia kwa pande zote, haswa katika mazingira haya maalum ya hapa. Tunaamini kwamba kuimarisha afya ya moyo na saikolojia ni muhimu zaidi kuliko kujenga hospitali tu."

    Lakini balaa liliibuka, mnano tarehe 4 Aprili mwaka 2011, Juliano Khamis aliuawa kwa kupigwa risasi na mwanamume mmoja karibu na Ukumbi wa Uhuru. Ingawa Palestina na Israel zilifanya uchunguzi wa tukio hilo la mauaji, lakini mpaka sasa bado matokeo ya uchunguzi huo hayajatangazwa.

    Mwaka mmoja baada ya kifo cha Khamis, Ukumbi wa Uhuru ulikumbwa na machafuko. Jeshi la Israel liliwakamata karibu nusu ya wafanyakazi wa ukumbi kwa kisingizio cha kufanya uchunguzi, na aliyeanzisha ukumbi huo Zakaria Zubeidi pia alizuiliwa nyumbani kwake huko Ramallah. Bw. Stanczak anasema:

    "Wakati ule usimamizi wa ukumbi ulikuwa na changamoto kubwa, hata haukuweza kudumu. Ilituchukua muda mrefu kusimama tena, na ili kuweza kufanya kazi kwa kuaminiwa ilichukua muda mrefu zaidi."

    Kiongozi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa watoto na vijana kwenye ukumbi huo Bw. Ahmead Tobasi anasema, wanatarajiwa kutoa jukwaa kwa vijana na wasichana wanaoishi katika kambi za wakimbizi, kuwawezesha kueleza hasira na masikitito yao kwa kutoa uvumbuzi, yaani njia zisizo za kimabavu.

    "Tunaamini kuwa watoto ni mustakabali wetu. Baada ya miaka kumi au ishirini watakomaa, kuoa au kuolewa na kuzaa watoto, wakati ule wataelewa umuhimu wa ukumbi wetu na maana ya uhuru, watajua ni namna gani wanavyotakiwa kuwachukulia jamaa, basi mabadiliko yatatokea vilevile katika jamii nzima."

    Ingawa mabadiliko hayatatokea katika siku moja, lakini wasanii wa Ukumbi wa Uhuru wanaendelea kufanya juhudi kutumia maonesho yao kuwashawishi watu wanaoishi ndani na nje ya kambi ya wakimbizi kuanza kufikiria mambo kwa kina zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako