• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wamekuwa na tabia nzuri ya kusoma vitabu

    (GMT+08:00) 2016-04-27 20:54:41

    Jumapili iliyopita ilikuwa ni siku ya kimataifa ya usomaji wa vitabu, katika kipindi cha leo, tutazungumzia mabadiliko yaliyotokea kwenye tabia ya wachina ya kusoma vitabu.

    Takwimu zilizotolewa wiki iliyopita na kampuni ya Amazon kuhusu tabia ya usomaji vitabu nchini China zinaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wachina wamekuwa na tabia nzuri ya kusoma vitabu, zaidi ya asilimia 80 ya waliohojiwa wanasoma vitabu kwa wastani wa nusu saa kila siku, na Kutokana na maendeleo ya teknolojia ya dijitali, asilimia 84 ya wahojiwa walisema pia wanasoma vitabu ya kidijitali.

    Ripoti hiyo ilitolewa na kampuni ya Amazon kwa kushirikiana na shirika la habari la Xinhua la China baada ya kuwahoji watu elfu 11 katika miji zaidi ya 500 kote nchini China. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, zaidi ya asilimia 80 ya wahojiwa wanasoma vitabu kwa zaidi ya nusu saa kila siku, na asilimia 40 kati yao kwa wastani wanasoma kwa zaidi ya saa moja kila siku. Kwa upande wa aina za vitabu, vitabu vya fasihi, sayansi za kijamii na taaluma ya menejimenti vinapendelewa zaidi na wasomaji wa China. Naibu mkurugenzi wa kampuni ya Amazon nchini China Bw. Shi Jianjun amesema, uchunguzi huo pia umeonesha kuwa, watu wa umri tofauti na jinsia tofauti waliohojiwa hupendelea vitabu vya aina tofauti.

    "Kwa upande wa umri, wahojiwa waliozaliwa katika miaka ya 1960 na miaka ya 2000, haswa wale waliozaliwa miaka ya 1960, wanapendelea zaidi usomaji wa kina, na muda wanaotumia kwenye usomaji vitabu ni asilimia 12 zaidi kuliko wanaotumia kwenye mitandao mingine ya kijamii; kwa upande wa jinsia, wanaume wanapendelea zaidi usomaji wa kina. Wanaume husoma vitabu kwa ajili ya kutafuta fursa bora za ajira, au kuongeza ujuzi, na kwa wanaume, asilimia 32 ya usomaji vitabu ni kwa ajili ya lengo hilo,kwa upande wa wanawake, kiasi hiki ni asilimia 21."

    Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, usomaji wa kidijitali umekuwa mwelekeo wa kisasa usiogeuka, na pia umekuwa sehemu muhimu ya maisha ya wasomaji vitabu. Ripoti ya Amazon pia inasema, vitabu vya kidijitali vinapendwa na wasomaji wengi zaidi kutokana na bei nafuu, urahisi wa kubebwa na kutumiwa. Uchunguzi unaonesha kuwa, idadi ya wahojiwa waliosoma vitabu vya kidijitali imeendelea kuongezeka kwa miaka mitatu mfululizo, na kufikia asilimia 84, ambalo ni ongezeko la asiimia 6 kuliko mwaka uliopita. Aidha, asilimia 56 ya wahojiwa wanasema, vitabu vya kidijitali vimeongeza kiwango cha jumla cha usomaji wao, na asilimia 90 ya wahojiwa wanasema watasoma vitabu vingi zaidi vya kidijitali katika siku za baadaye.

    Kutokana na maendeleo ya vitabu vya kidijitali, uchapishaji wa vitabu vya karatasi na kiwango cha usomaji wa vitabu hivyo ni suala ambalo watu wengi wa sekta ya uchapishaji wana wasiwasi nalo, hata kulikuwa na watu waliotabiri kuwa "vitabu vya karatasi vitakufa". Akizungumzia kauli hiyo, naibu mkurugenzi wa kampuni ya Amazon nchini China Bw. Shi Jianjun amesema, idadi ya wasomaji wa vitabu vya kidijitali imeendelea kuongezeka siku hadi siku, lakini haimaanishi kuwa vitabu vya karatasi vitatoweka, na kinyume chake, vitabu vya aina hizo mbili vitahimizana.

    "Vitabu vya aina hizi mbili vinahimizana, na pia kuwa na nguvu ya pamoja. Asilimia 4 tu ya wahojiwa walituambia kwamba wanasoma vitabu vya karatasi tu na hawataki vitabu vya kidijitali, na asilimia 84 ya waliohojiwa wanasema, wanasoma vitabu vya aina zote mbili. Kwa kupitia mitindo tofauti ya karatasi na dijitali, vitabu vya aina hizo mbili vimewapatia wasomaji wetu uzoefu kamili wa usomaji, na katika hali tofauti, unaweza kuchagua njia inayofaa zaidi ya kusoma vitabu."

    Katika hali ya sasa, haijalishi ni vitabu vya karatasi au vya kidijitali, vitabu vinavyonunuliwa kwa wingi huwa ni chaguo la kwanza kwa wasomaji wengi. Hata baadhi ya vijana wanapochagua vitabu, kitu cha kwanza wanachoangalia ni orodha ya vitabu vinavyonunuliwa kwa wingi. Akizungumzia hali hiyo, profesa Chen Pingyuan wa chuo cha fasihi katika chuo kikuu cha Beijing amependekeza kuwa, wasomaji wanapaswa kuzingatia zaidi vitabu vizuri ambavyo havinunuliwi sana.

    "Vitabu vinavyonunuliwa zaidi vinawakilisha tu upendeleo wa kisanii na uwezo wa usomaji wa watu wa kawaida, kitabu kinachochukua nafasi ya kwanza kwenye orodha ya mauzo si lazima kiwe kitabu kizuri, lakini kuna vitabu vingi vizuri ambavyo havinunuliwi sana. Tunapaswa kutafuta na kugundua vitabu vile vizuri visivyojulikana na umma ambavyo haviko kwenye orodha ya mauzo, na kuvifahamisha kwa watu ili wavisome."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako