• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waamua kuimarisha juhudi za kujenga amani

    (GMT+08:00) 2016-04-28 09:37:05

    Picha:MONUSCO / Abel Kavanagh

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja huo wamepitisha azimio la kuimarisha juhudi za kujenga amani ya kudumu, na kutoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono kazi hizo.

    Azimio hilo limesisitiza kuwa "utimizaji wa amani ya kudumu" sio tu ni lengo bali pia ni mchakato unaojumuisha hatua mbalimbali nyingi zikiwemo kuzuia migogoro, kuondoa vyanzo vya matatizo, kusaidia usimamishaji vita, kuhimiza maridhiano ya kitaifa na kufanya ukarabati.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon ametoa taarifa akikaribisha kupitishwa kwa azimio hilo na kutaka nchi mbalimbali kutoa msaada kwa nchi zilizokumbwa na migogoro.

    Wakati huohuo balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi amesema ufuatiliaji unapaswa kuwekwa katika kushughulikia umaskini, kukosekana kwa maendeleo na matatizo mengine yanayosababisha vita na misukosuko, na ametoa mwito wa kufanya juhudi kuzisaidia nchi zilizoathiriwa na migogoro kupata ujenzi mpya katika sekta mbalimbali, na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako