• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maelfu wa watu wa Afrika Kusini wamtaka rais Zuma kujiuzulu

    (GMT+08:00) 2016-04-28 09:42:34

    Maelfu wa watu wa Afrika Kusini wameandamana kumtaka rais Jacob Zuma kujiuzulu.

    Watu hao wakiongozwa na mashirika 75 ya kiraia, wametoa matakwa hayo kufuatia uamuzi uliotolewa tarehe 31 Machi na mahakama ya katiba, unaosema kuwa Rais Zuma hakufuata mapendekezo ya msimamizi wa mali za umma ya kumtaka kulipia gharama za marekebisho ya nyumba yake binafsi huko Nkandla, KwaZulu-Natal, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka katiba.

    Maandamano yamefanyika nchini kote ikiwemo mjini Johannesburg, Cape Town na Durban. Mjini Johannesburg, mamia ya waandamanaji wakiwemo wasomi, wanasiasa, walinzi wa mazingira, wanafunzi, wafanyabiashara na wanaharakati wa kijamii wakimtaka rais Zuma ajiuzulu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako