• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  Bi.Li Chunfeng na supermarket yake ya upendo

    (GMT+08:00) 2016-05-05 15:21:27

     

    Leo tutazungumzia mwanamke mmoja wa kawaida na supermarket yake ya upendo. Jina la mwanamke huyu ni Li Chunfeng, ambaye ni mwanakijiji wa kawaida wa kijiji cha Shibeng mkoani Henan. Bibi huyu ameshikilia kufanya shughuli za hisani kwa miaka 36, ambapo kila siku anaainisha na kugawa nguo kwa walemavu wa viungo, walemavu wa akili na watu maskini vijijini. Hadi sasa amegawa nguo zaidi ya elfu kumi.

    Katika ofisi ya kamati ya wanakijiji ya kijiji cha Shibeng, Bi. Li Chunfeng alikuwa anachambua nguo zaidi ya 200 zilizotolewa na wafanyakazi wa shirikisho la hisani la Xingyang, Henan. Kwa kuwa Bi Li ana umri mkubwa, baada ya kuchambua nguo kwa muda, jasho lilimtoka.

    "Baadhi yao ni walemavu wa akili, na baadhi yao walikabiliwa na pigo kubwa kwenye familia na hivyo kuwasababishia matatizo ya kiakili, ambao hawajali wanavaa nguo au la. Nataka kuwapatia nguo ili wavae nguo kama sisi, na kuishi kwa usawa pamoja nasi. "

    Kijiji cha Shibeng ni kijiji maskini. Mwaka 2008 Bi. Li Chunfeng alianzisha supermarket moja katika ofisi ya kamati ya wanakijiji ya kijiji hicho, ambapo anakusanya na kuchambua nguo na bidhaa nyingine za matumizi zilizotolewa na pande mbalimbali, na kuzigawa kwa watu wenye matatizo ya kiuchumi na wasiojiweza kimaisha wa kijiji chake na vijiji jirani. Bibi Fan wenye umri wa miaka 72 ni mwanakijiji wa kijiji cha Shibeng, ambaye anamfahamu Bi. Li Chunfeng kwa miaka kadhaa. Kutokana na matatizo ya kiuchumi, Bibi Fan anakwenda supermarket ya Li Chunfeng mara kwa mara kuchukua nguo. Anasema,

    "Li Chunfeng ni mtu mwema sana. Hapa tunaweza kuchagua nguo tunazopenda. Kuna nguo za aina mbalimbali. Yeye anafanya mambo mengi ya kuwasaidia wengine. Anawapa nguo walemavu kijijini. Si rahisi kwake kushikilia kufanya shughuli za hisani. Ni kama familia moja, yeye anawaangalia watu maskini kila mwaka kama vile anawaangalia watoto wake."

    Kuna zaidi ya familia 20 zenye watu zaidi ya 80 maskini kama Bibi Fan waliosaidiwa na Li Chunfeng katika kijiji cha Shibeng. Kwa sababu Bi. Li Chunfeng ameshikilia shughuli za hisani kwa miaka kadhaa bila kusita, wanakijiji wote wanamsifu sana.

    Miaka 36 iliyopita, kwa mara ya kwanza Bi. Li Chunfeng alifanya shughuli za hisani. Majira ya baridi ya mwaka 1980, siku ya tatu tu baada ya arusi yake, Bi. Li Chunfeng alipomwona Bibi Jin mwenye matatizo ya kiakili amevaa nguo nyepesi na kutetemeka kwa baridi huku akitembelea na mtoto wake mtaani, Bi. Li Chunfeng mara moja alirudi nyumbani na kuchukua nguo mpya mbili na kumpa Bibi Jin. Alimwambia mume wake kuwa, Bibi Jin ana matatizo ya kiakili, ambaye hawezi kujitunza na kumtunza mtoto wake, hivyo anataka kumsaidia.

    Kuanzia wakati huo, kila mwaka wakati wa mabadiliko ya majira Bi. Li Chunfeng anatoa nguo, kwa wanakijiji wenye matatizo ya kiuchumi, wakati wa sikukuu yeye anawapatia watu walemavu kijijini mafuta na unga. Kwa sababu familia ya Bi. Li Chunfeng inashughulikia biashara ya uchukuzi wa vifaa vya ujenzi, hivyo hali ya maisha ya familia ya Li Chunfeng ni nzuri zaidi kuliko wanakijiji wengine. Ingawa wakati wingine shughuli za hisani zinaweza kuathiri biashara ya familia yake, lakini Bi. Li Chunfeng hajaacha shughuli hizo. Anasema,

    "Kama nisingefanya shughuli za hisani, katika miaka kumi kadhaa iliyopita ningeweza kupata yuan milioni moja hivi. Lakini wakati ninapoona watu hao wenye matatizo ya kiuchumi, hasa walemavu wa akili na wasiojiweza kimaisha, nataka kuwasaidia ninavyoweza, hata kama biashara yetu itaathirika. Wakati ule nilikuwa sifahamu maana ya hisani, nilitaka kuwasaidia tu, ili waweze kuishi vizuri."

    Mwaka 2004 mtoto wa Li Chunfeng alikwenda mjini Zhengzhou na kuishi mjini humo. Wakati alipomtembelea mwanawe, Li Chunfeng aligundua watu wengi mijini hutupa nguo baada ya kuzivaa kwa muda fulani, lakini kwenye maskani yake kuna watu wengi walio na upungufu wa nguo na chakula, hivyo alitaka kukusanya nguo kutoka mijini na kuzileta kijijini. Alinunua mkokoteni na kwenda soko la Zhengzhou kukusanya nguo zilizotumika. Lakini kukusanya nguo zilizotumika mitaani kumeleta shinikizo kubwa kwake. Anasema,

    "Baadhi ya watu hawanielewi, wao waliniuliza natoka wapi, sikuthubutu kuwaambia natoka wapi. Nilikuwa naogopa wangesema mimi ni mdanganyifu."

    Siku moja wakati Li Chunfeng alipokusanya nguo zilizotumika sokoni, mzee mmoja alimgombeza sana, alimsema Li Chunfeng na kumtuhumu kuwa ni mdanganyifu. Li Chunfeng alilia sana. Anasema,

    "Sikulia kwa miaka mingi, lakini siku hiyo nililia sana. Yeye alinigombeza na kunituhumu kuwa ni mdanganyifu."

    Lakini Li Chunfeng bado alishikilia kwenda sokoni na kukusanya nguo zilizotumika, kwani zaidi ya watu 80 kijijini wanahitaji nguo hizo. Baadhi ya watu hawakuamini kwamba yeye alinunua guo zao zilizotumikwa kwa ajili ya hisani. Baada ya mwaka mmoja, watu wengi zaidi walianza kufahamu hali yake, na walianza kumpa nguo zilizotumika bila malipo.

    Licha ya supermarket ya upendo kwenye kijiji cha Shibeng, idara ya mambo ya raia ya mji wa Xingyang pia imeanzisha supermarket ya upendo kwenye tarafa ya Jiayu, ambayo pia inaendeshwa na Li Chunfeng, ili watu wa vijiji na tarafa nyingine waweze kupata nguo zilizotumika. Naibu mkurugenzi wa idara ya mambo ya raia ya Xingyang Bw. Ma Jiangtao anasema,

    "Nilishangaa sana baada ya kufahamu hali ya Li Chunfeng, kwani alianza kufanya shughuli za hisani miaka zaidi ya 30 iliyopita. Ameongoza watu wengi kufanya shughuli za hisani. Kwa sababu ya Li Chunfeng, wanakijini wengi wana njia ya kuwasaidia watu wanaohitaji msaada. Ameeneza upendo kati ya watu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako