• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asisitiza umhimu wa kutekeleza mtizamo wa usalama wa Asia kwenye mkutano wa CICA

    (GMT+08:00) 2016-04-28 16:07:16

    Kikao cha tano cha mawaziri wa mambo ya nje cha Mkutano kuhusu maingiliano na hatua za kujenga uaminifu barani Asia kimefanyika leo hapa Beijing.

    Akihutubia kwenye ufunguzi wa kikao hicho Rais Xi Jinping wa China , amesisitiza umuhimu wa kushikilia na kutekeleza mtizamo wa usalama wa Asia, na kuhimiza ujenzi wa mfumo wa usimamizi wa kiusalama wenye umaalum wa Asia.

    Rais Xi amesema, ushirikiano wa kiusalama barani Asia unapaswa kuimarishwa zaidi, na nchi za Asia zina uwezo na vilevile mahitaji ya kulinda mazingira ya kiusalama na kimaendeleo barani humo kwa njia ya mazunguzmo na ushirikiano.

    "Nchi za Asia siku zote zina tabia ya uwazi na ushirikishaji, na pia zina busara zenye upeo wa mbali. Tunakaribisha nchi zilizoko nje ya kanda hii zitoe mchango kwa ajili ya amani na maendeleo ya Asia, na kushirikiana na nchi za Asia katika kuhimiza usalama, utulivu, maendeleo na ustawi wa bara hili. Asia yenye utulivu na maendeleo inanufaisha dunia nzima, na Asia yenye vurugu na ghasia, pia italeta madhara kwa dunia."

    Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, hotuba hiyo ya rais Xi Jinping inaonesha mchango mwingine muhimu uliotolewa na China baada ya kutoa mtizamo wa usalama wa Asia kwenye mkutano wa kilele wa CICA uliofanyika mjini Shanghai mwezi Mei mwaka 2014. Amesisitiza kuwa mkutano huu utahimiza maendeleo ya mchakato wa kukuza maingiliano na kuimarisha uaminifu kati ya nchi za Asia, kupanua mazungumzo na ushirikiano wa kiusalama barani Asia, na kufanya juhudi za kiujenzi katika kulinda amani, usalama na utulivu wa kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako