• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China ahutubia kwenye kikao cha tano cha CICA

    (GMT+08:00) 2016-04-28 16:43:31

    Kikao cha tano cha mawaziri wa mambo ya nje cha mkutano kuhusu maingiliano na hatua za kujenga uaminifu wa nchi za Asia CICA umefanyika leo hapa Beijing, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameendesha na kuhutubia mkutano huo.

    Bw. Wang Yi amesema, kwenye hotuba ya rais Xi Jinping wa China alitoa maoni na mapendekezo ya China kuhusu namna ya kutekeleza mtizamo wa usalama wa Asia na kujenga mfumo wa usimamizi wa kiusalama wenye umaalumu wa Asia. Amesema Huo ni mchango mwingine muhimu uliotolewa na China baada ya kutoa mtizamo wa usalama wa Asia kwenye mkutano wa kilele wa CICA uliofanyika mjini Shanghai mwezi Mei mwaka 2014, na kwamba mkutano huo utahimiza maendeleo ya kina ya mchakato wa kuhimiza maingiliano na kujenga uaminifu wa Asia, kupanua mazungumzo na ushirikiano kuhusu usalama barani Asia, na kufanya juhudi za kiujenzi katika kulinda amani, usalama na utulivu wa kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako