• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifaa vilivyotolewa na China kwa Ecuador vyawasili

    (GMT+08:00) 2016-04-28 17:58:12

    Ndege nne za vifaa vilivyotolewa na China kwa ajili ya kusaidia kwenye shughuli za uokozi nchini Ecuador ambayo ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi vimewasili jana nchini humo.

    Msaada huo umejumuisha vifaa mbalimbali vikiwemo mahema elfu 5,400 na vitanda vya kukunja elfu 9,999. Akipokea vifaa hivyo kwenye uwanja wa ndege wa Ecuador makamu wa kwanza wa rais Rossana Alvarado aliishukuru serikali ya China kwa msaada huo, akisema vitasaidia kuwahifadhi waathirika wakati ujenzi wa sehemu zilizoathirika na tetemeko ukiendelea.

    Naye balozi wa China nchini Ecuador Wang Yulin amesema nchi yake ilishtushwa na janga hilo na kupitia msaada huo China inapenda kuonesha mshikamano wake na serikali ya Ecuador na watu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako