• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapitisha sheria ya usimamizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya nje

    (GMT+08:00) 2016-04-28 18:24:43

    Bunge la umma la China leo limepitisha sheria kuhusu usimamizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya nchi za nje, ambapo mashirika hayo yanatakiwa kuidhinishwa na mamlaka ya China kabla ya kuanzisha shughuli zao katika China bara.

    Kwa mujibu wa sheria hiyo, mashirika ambayo yanataka kuanzisha ofisi zao za kudumu au za muda yote yanatakiwa kuomba idhini kutoka kwa mamlaka ya China.

    Wizara ya usalama wa umma ya China na idara za polisi za mikoa mbalimbali zitawajibika na kazi ya usajili na usimamizi. Mashirika yasiyo ya kiserikali ya nchi za nje yatakayofanya kazi bila ya kupatiwa idhini yataadhibiwa.

    Sheria hiyo inalenga kuweka vigezo kwa shughuli za mashirika hayo nchini China, kulinda haki na maslahi yao na kuhimiza maingiliano na ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako