• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa UN asema ratiba ya mazungumzo ya amani kuhusu Syria bado haijamuliwa

    (GMT+08:00) 2016-04-28 18:33:15

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Staffan de Mistura leo amesema, mazungumzo ya amani ya kipindi cha pili kuhusu suala la Syria yaliyoanza tarehe 14 Aprili huko Geneva yamemalizika tarehe 27 kwa mujibu wa mpango uliowekwa hapo awali, hata hivyo amesema ratiba ya mazungumzo ya kipindi kijacho bado haijaamuliwa.

    Bw. De Mistura amesema mazungumzo ya kipindi cha pili hayakuwa ya utaratibu, lakini ujumbe wa serikali ya Syria, ujumbe wa wapinzani wakubwa nchini humo, wajumbe wa wanawake wa Syria na makundi husika ya kisiasa wote wameeleza nia ya kutatua mgogoro kwa njia ya siasa, na pia wamefikia maoni ya pamoja kuhusu mchakato wa mpito wa kisiasa na uundaji wa serkali ya mpito.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako