• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Singapore kutumia bandari ya Dar es Salaam kuwa kiunganishi cha biashara EAC

    (GMT+08:00) 2016-04-28 20:36:45

    Waziri wa biashara na viwanda wa Singapore Bw Koh Poh Koon amesema nchi yake inapanga kutumia bandari ya Dar es Salaam kama kiunganishi cha biashara kati ya nchi hiyo na mataifa mengine ya Afrika Mashariki (EAC).

    Akizungumza kwenye mkutano na waziri mkuu wa Tanzania Bw Kassim Majaliwa, Bw Koo amesema Singapore iko tayari kutoa fursa kwa wataalamu wa Tanzania kwenda kufanya kazi katika Bandari ya Singapore ili kupata uzoefu utakaosaidia uendeshaji wa bandari za Tanzania.

    Aidha Koon ambaye pia alikuwa ameandamana na wafanyabiashara 40 kutoka Singapore, amesema kampuni ya Hyflux ya Singapore tayari imeanza kuwekeza nchini humo kwa kujenga eneo maalumu la uchumi mkoani Morogoro, ambapo ndani ya kipindi cha miaka mitano wanatarajia kujenga miundombinu wezeshi ya kuweka viwanda vya kati, maeneo ya biashara na nyumba za makazi zipatazo 37,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako