• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watano wafariki, na zaidi ya elfu 13 kukosa makazi katika mafuriko Tanzania

    (GMT+08:00) 2016-04-28 20:44:07

    Mvua kubwa zinazoendelea katika mkoa wa Morogoro pamoja na mafuriko zimesababisha vifo vya watu watano na wengine zaidi ya elfu 13 kukosa makazi.

    Vifo hivyo vya watu watano vimepelekea idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko kufikia 13 ndani ya wiki moja tu, baada ya watu wengine wanane kufariki katika mkoa wa Kilimanjaro na kuacha mamia ya watu kukosa makazi. Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steve Kebwe amesema hivi sasa wanatafuta misaada ya kibinadamu kutoka kwa wadau mbalimbali, akisistiza kuwa misaada hiyo ni muhimu kwa sasa kwani waathirika hawana mahali pa kuishi, chakula wala dawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako