• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto kuendelea kupata usaidizi na taasisi za fedha

    (GMT+08:00) 2016-05-03 06:34:17

    Huku idadi ya watoto maskini wenye kiu ya masomo ikiongezeka barani Afrika, mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali zikiwemo taasisi za kifedha yameanza kuunga mkono jamii kwa kutoa msaada wa masomo kwa watoto hao ili kuhakikisha wanapata fursa ya kuwa na maisha mazuri katika siku za baadaye.

    Umaskini ukiendelea kushuhudiwa nchini Kenya, na uwezo wa kulipa karo za shule ukuendelea kudidimia. Mashirika tofauti yameingilia katika na kujitolea kusomesha watoto. Benki kadhaa nchini ikiwemo first community bank zimejitolea kufadhili watoto wasio jiweza kimasomo. Seneta wa Mandera Bw: Billow Kerrow alipongeza hatua hiyo.

    "Nataka kushukuru benki hii kwa kuanzisha wakfu ya kusaidia wanafunzi wasiojiweza, kwa sababu hali kama hii imeonekana kuongezeka mno pale wazazi hawawezi kulipia karo watoto wao"

    Aidha aliziomba taasisi zengine ziinge mfano huu, ili tupunguze umaskini nchini.

    "Hii fursa ni muhimu sana, na ndio maana taasisi kama hizi, first community bank na taasisi zengi ziko jukumu la kusaidia wasio jiweza kimaisha na maskini katika jamii"

    Kupitia mkutano huu bw Billow Kerrow aliomba serikali za kaunti kuwekeza kwa ajili ya elimu ya watoto.

    "Ni vyema serikali za kaunti ziwekeze maelfu ya milioni ya fedha katika elimu, kwa sababu hakuna kitu muhimu kama kusomesha watu wetu"

    Binti Mmoja ambaye alivuma kwa magazeti na runinga za humu nchini miaka miwili iliyopita, ni mmoja tu wa wanafunzi ama watoto ambao wamefaidika na wakfu hii ya elimu. Dada huyu ambaye anayejulikana kama Joyce shida zake zilianza wakati alipokataa kufanyiwa ukeketaji na kuozwa mapema.

    Bwana Wekesa mwakilishi wa watoto, anasema ni vyema benki ama mashirika mengi ya kiserikali na yasiyo yakiserikali kuwekeza kwa elimu ya watoto badala ya kuweka pesa kwa watoto.

    "Nataka kushukuru benki hii kwa kuchukua hatua ya kusaidia watoto wetu, kama nilivyosema awali nimekuwa mwakilishi wa watoto, na tumeona shida nyingi watoto upitia, hivyo nifuraha yetu kuona benki zikiwekeza kwa elimu ya watoto badala ya kuweka pesa kwa watoto"

    Kupitia msaada huu wa benki ya first community wameweza kufadhili watoto wapatao 81, ambao walipata alama 350 na mtihani wao mwisho. Na isitoshe benki hiyo imesema inataka kuongeza idadi hiyo ya wanafunzi hadi wanafunzi 800,000, kwani ndio wataka inua uchumi wa Kenya siku za baadaye.

    "Tunataka kuongeza namba ya wanafunzi kutoka 81 hadi 800,000, nchini kote, kwani shilingi moja ama dola moja yeyote inayo tumiwa kuelimisha mtoto itaongeza asilimia 20 hadi 25 kwa uchumi wa nchi baadaye"

    Afisa katika benki hiyo anasema mpango huu ni wakupatia watoto karo za shule lakini wanapanga kupiga hatua nyengine ya kuwapa watoto pesa za matumizi.

    "Tumeanza mpango wakuwafadhili watoto kimasomo kwa kuwapatia karo lakini hatutaki kuwachi hapo kwani twataka kuwapa pia pesa za matumizi"

    Profesa Abdul Essaji, mjumbe wa bodi katika benki hiyo anasema.

    "FCB, ni benki inayojulikana kama benki ya kislam, benki hii haitoi fadhila kwa watoto hawa bali watoto hawa ndio wanaotoa hisani kwa benki hii kwa kuwapatia fursa ya kuwa sehemu ya maisha yao na pia kubadili maisha yao. "

    Aidha aliongeza kwa kusema kando benki hii kuwa ya kislam haichangui dini, rangi ama kabila, inahudumia kila mtu.

    "Tunakubali watu wote bila kujali dini, rangi, na pia kabila, na kweli kuna ushahidi tosha kwamba FCB hata kama inahudumia wanao amini dini ya kislam, pia inahudumia watu wa dini zengine, hapa leo kuna mchanganyiko watoto wa kislam na wale siwakislam"

    Gavana wa kaunti ya garissa bw: Nathifu jama amehaidi kusomesha watoto wawili mwaka ujao.

    "Najitolea kuchukua wanafunzi wawili ambao watafanya vizuri katika mtihani mwaka huu wa KCPE na tuhakikishe tumelipa karo yote ya shule ya upili hadi wamalize"

    Serikali imeomba taasisi na mashirika tofauti kuanza mipango kama hii kupunguza umaskini, katika jamii.

    Na pia watoto wanaombwa na mashirika yanayo pingania haki za watoto kuwasiliana nao wakati wowote wanajambo ambalo linaweza kurudisha nyuma uchumi wakenya ikiwemo ukosefu wa karo, ukeketaji na ndoa za mapema.

    Asante sana Serah Nyakaru kwa ripoti hiyo. Msikilizaji, mara nyingi wazazi au walezi wanajiuliza, ni urithi gani wanaweza kuwaachia watoto wao? Wengine wanakusanya mali, wengine huwawekea akiba, na mambo mengine mengi. Hayo yote ni sawa. Lakini kitu ambacho unaweza kumwachia mtoto wako, pamoja na hayo mengine, ni elimu, kwani elimu ndio itamwezesha kuendeleza na kuzalisha zaidi kile utakachomwachia. Kwa mtazamo huo, tuwekeze zaidi kwenye elimu kwa watoto wetu, kwani kama unavyosema msemo huu, "urithi pekee unaoweza kumwachia mtoto wako ni elimu"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako