• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uvumbuzi wawa njia moja muhimu kwa makampuni ya China kupanua soko nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2016-05-04 12:50:07


    Takwimu mpya zinaonyesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu, hali ya kupungua kwa biashara ya China na nje imeanza kuboreshwa, pamoja na kuwa uuzaji bidhaa za China nje ya nchi katika mwezi Machi ulipata ongezeko hasi katika miezi 9 iliyopita. Makampuni ya China yako tayari kukabiliana na mazingira haya mapya, na mengi yao yanafanya mageuzi na uvumbuzi katika sekta za teknolojia, muundo na usimamizi, na nguvu mpya za kukuza biashara ya nje ya China zimeanza kuonekana. Kufanya mageuzi ya utoaji kwa uvumbuzi, kuongeza thamani ya nyongeza ya bidhaa na kuboresha muundo wa biashara ya nje ni miongoni mwa njia mpya zinazotumiwa na makampuni ya China kupanua masoko nje ya nchi.

    Kabla ya mwaka mmoja uliopita, bosi wa kampuni ya teknolojia ya habari ya Zhiyu mkoani Zhejiang Bw. Ding Wei alishughulikia uuzaji wa bidhaa za jadi nje ya nchi. Lakini kutokana na kupungua kwa uchumi wa dunia, biashara ya nje ya China inazidi kukabiliwa na changamoto kubwa, kwa hiyo Ding alifanya mageuzi na kuanza kuuza nguo za wanawake katika mtandao wa internet unaovuka mipaka ya nchi. Akifafanua wazo lake la ubunifu, Ding anasema,

    "Katika miaka hii miwili, maduka makubwa ya jadi ya Marekani kama vile Wal-Mart, Macy's au Target yamefunga maduka mengi, lakini wakati huohuo makampuni ya Marekani yanayouza bidhaa katika mtandao wa internet yameongezeka kwa asilimia 18, mengi yao yamefungua vituo vya manunuzi nchini China, na wauzaji wa China wanachukua asilimia kubwa katika tovuti zao, idadi ambayo ni kati ya asilimia 40 hadi 60."

    Baada ya kulenga soko kwa usahihi, kampuni ya Ding ilikua kwa kasi, na sasa imejenga uhusiano wa ushirikiano na makampuni zaidi ya 1,200 ya nchini China, na pia maduka yake ya kwenye tovuti yako katika nchi na sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo Marekani na Ulaya. Mwaka jana aliuza bidhaa milioni 10 na biashara ilifikia dola za kimarekani milioni 100.

    Kuachana na muundo wa jadi wa kibiashara na kufuata njia ya uchumi wa kiteknolojia vimewezesha makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati ya China kushiriki katika ushindani wa kimataifa. Lakini je, kwa yale ya jadi ya uzalishaji, watawezaje kukabiliana na changamoto mpya za biashara ya nje?

    Kabla ya miaka kumi iliyopita, kampuni ya Chunfeng ilikuwa inashughulika na uzalishaji wa jadi wa spea muhimu za pikipiki na gari zima. Mwaka 2008, kampuni hiyo ilifanya mageuzi na kuamua kutengeneza pikipiki ya kimichezo yenye kiwango cha juu duniani. Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni hiyo Lai Guogui anasema,

    "Wakati ule tuliona kuwa pikipiki ya michezo na burudani itakuwa ni mwelekeo wa maendeleo katika siku za baadaye, hivyo tulianza kujiandaa kutengeneza vifaa kama vile pikipiki yenye magurudumu manne, na magurudumu mawili, pikipiki ya kiburudani ni mkakati na lengo letu, halafu tukaweka mkazo kuinua ngazi na ubora wa bidhaa zetu."

    Lakini kama wangeendelea kutumia mbinu za jadi za uzalishaji, wangeshindwa kupunguza gharama na kuinua ufanisi, na ni vigumu kuingia kwenye masoko ya Ulaya na Marekani. Kwa hiyo walipobadilisha mashine yao waliagiza mfumo wa uzalishaji wenye teknolojia ya hali ya juu, na pia kutengeneza pikipiki kwa mujibu wa mahitaji ya wateja. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Gao Qing anasema, baada ya kuunganisha bidhaa zao na mtandao wa internet, ufanisi wa uzalishaji umeongezeka na bidhaa zao zinakidhi mahitaji ya nchi tofauti, na masoko yao katika nchi za nje yameongezeka kwa kasi.

    "Baada ya mfumo mzima kuboreshwa, ufanisi na muda wa usanifu wa bidhaa uliongezeka. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2014, kiwango cha mzunguko wa bidhaa zinazohifadhiwa kwenye ghala kimeongezeka kwa asilimia 50, kiwango cha matumizi ya mashinde kiliongezeka kwa asilimia 25, kiwango cha uzalishaji kiliongezeka kwa asilimia 30 na muda wa usanifu wa bidhaa ulifupishwa kwa asilimia 30. Na biashara yetu katika soko la Marekani pia iliongezeka kwa mara moja na asilimia 20 katika soko la Ulaya."

    Kama ilivyokuwa kampuni ya Chunfeng, kampuni ya Zhengtai ilikuwa kiwanda cha jadi cha kuzalisha vifaa vya umeme, lakini tofauti ni kuwa baada ya kufanya mageuzi ya ubunifu, kampuni hiyo siyo tu imeboresha shughuli zake za kiviwanda, bali pia ushawishi wake umeongezeka katika sekta ya nishati mpya duniani. Mwenyekiti wa kampuni hiyo Nan Cunhui amesema katika miaka ya hivi karibuni, kampuni yake imetengeneza vifaa vya kuzalisha umeme, kusambaza umeme, kubadilisha mkondo wa umeme, kuratibu umeme na kutumia umeme katika vifaa vya teknolojia ya kisasa, nishati mpya na teknolojia ya habari. Amesema kampuni ya Zhengtai inabadilisha njia iliyotumia zamani ya kuuza bidhaa tu.

    "Zamani tuliuza bidhaa tu, lakini baada ya kufanya uwekezaji, sasa tunalipwa ada za umeme, yaani kuuza huduma. Hayo ni mageuzi tunayofanya kutoka sekta ya uzalishaji hadi sekta ya huduma."

    Kwa mtazamo mpya wa kibiashara, kampuni ya Zhengtai inachukua "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kama fursa na njia muhimu kwa makampuni ya China kufanya ushirikiano wa kiviwanda wa kimataifa na uzalishaji wa vifaa, kuweka mkazo masoko katika nchi zinazohusishwa na Ukanda huo, na pia kuingia kwenye soko la Ulaya na Marekani. Bw. Nan Cunhui anasema,

    "Zhengtai imezindua mradi mjini Xi'an, magharibi mwa China, ambako ni mwanzo wa 'Ukanda Mmoja na Njia Moja', halafu tulifuata Ukanda na Njia hiyo. Tumeshirikiana na kampuni nyingine ya kiserikali kuwekeza dola za kimarekani milioni 500 nchini Combodia na kujenga mabwawa matatu na kutoa asilimia 50 ya umeme unaohitajika katika mkoa wa Koh Kong. Nchini Korea Kusini, Thailand, India, Italia, Hispania, Bulgaria, Romania na Marekani, pia tumejenga vituo 30 vya kuzalisha umeme kwa jua."

    Mwenyekiti wa kampuni ya Chunfeng Lai Guogui amesema, ubora ni muhimu zaidi kwa bidhaa, pia ni jambo linaloamua kama bidhaa zinazozalishwa nchini China zitapata soko nje ya nchi.

    "Makampuni yanayotengeneza bidhaa bora yanaweza kupata faida, kama tunatengeneza bidhaa kwa bidii kama fundistadi, makampuni yetu yana mustakbali mzuri."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako