• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shule aliyosoma William Shakespeare yaadhimisha miaka 400 tangu kifo chake

    (GMT+08:00) 2016-05-04 15:46:16

    Tarehe 23 mwezi Aprili mwaka huu ilikuwa ni maadhimisho ya miaka 400 tangu kifo cha mtunzi mashuhuri wa opera wa Uingereza William Shakespeare. Katika kipindi cha leo, tutatembelea kwa pamoja maskani yake na shule alizosoma katika mji wa Stratford ili kufahamu historia ya maisha yake alipokuwa kijana.

    Katika kuadhimisha miaka 400 ya kifo cha William Shakespeare, tarehe 23 Aprili shule ya mfalme Edward VI aliyosoma ilifungua kwa umma madarasa na ukumbi wa mji vilivyokarabatiwa upya kwa mapambo ya mtindo wa asili wa Tudor.

    Bi. Mairi Macdonald ni mtaalamu wa utafiti wa mabaki ya kale wa Shirika la mfuko wa makazi ya asili ya William Shakespeare. Anasema,

    "Watalii wanaokuja kutembelea hakika watavutiwa sana. Tulifanya utafiti wa madarasa ya enzi yake na kuyalinganishana ili kujua tofuati kati yao, kwa njia hii tumerejesha hali ilivyokuwa ya darasa alilosoma William Shakespeare, ikiwemo meza na kiti, na jinsi vilivyopangwa. Hii ni fursa nzuri ya kufahamu elimu ya darasani katika enzi ya Tudor."

    Bi. Mairi Macdonald amesema, ingawa hakuna rekodi halisi za kihistoria, lakini wanataaluma wamekubaliana kwamba, William Shakespeare alianza kusoma katika shule ya mfalme wa Edward VI alipokuwa na umri wa miaka 7 hivi, na shule hiyo ilikuwa ndani ya ukumbi wa mji ambao ni jengo la kale zaidi huko Stratford. Mwezi Julai mwaka jana, kutokana na juhudi na maandalizi ya shule ya mfalme wa Edward VI, ukumbi wa mji wa Stratford ulikarabatiwa na kupambwa upya, mradi ambao uligharimu pound milioni 1.8.

    Bi. Mairi Macdonald amesema, mradi huo mkubwa wa ukarabati una umuhimu maalumu kwa mji huo mdogo wa Stratford.

    "Katika kipindi cha miaka 50 ijayo, hatutafanya maadhimisho makubwa ya William Shakespeare kama haya. Kama tukitaka kupanga au kuandaa miradi mikubwa inayohusiana na William Shakespeare, hii labda ni fursa ya mwisho kwa watu wa kizazi changu katika maisha yetu. Kwa hiyo kukamilika kwa mradi huo kuna umhimu maalumu."

    Ukumbi wa mji wa Stratford uliofunguliwa kwa umma utaendelea kuwa mahali pa elimu inayotumika na shule ya mfalme wa Edward VI. Watalii wanaruhusiwa kuingia alasiri kila siku, na kufahamu elimu iliyotolewa katika enzi ya Tudor kwa kupitia rekodi za sauti au video.

    Mtafiti kuhusu William Shakespeare, Prof. Ronnie Mulryne wa chuo kikuu cha Warwick anasema, kufunguliwa kwa shule na darara alilosoma William Shakespeare kunaweza kuhamasisha vijana wengi zaidi kumfahamu mtunzi huyo mkubwa wa opera na kazi zake.

    "Wakati wanajihisi mazingira aliyosoma Shakespeare, na kufikiria kwamba Shakespeare alipokuwa na umri kama wao, kwa kufanya bidii alikuwa mwandishi na mtunzi opera, halafu akaenda London na kuwa mbia wa jumba la maonyesho ya sanaa, na kupata mafanikio na kujiendeleza kwa kutegemea uwezo wake, labda vijana wengi wa sasa wanaweza kufikiri ni vipi aliweza kufanikiwa na huenda wao wenyewe pia wanaweza kufanikiwa hivyo tu? Tunatumai kurejesha hali halisi ilivyokuwa katika enzi ya Shakespeare alipokuwa mwanafunzi kwa njia za burudani."

    Lakini, kuwa mwanafunzi katika enzi ya William Shakespeare kweli hakukuwa jambo rahisi.

    "Wakati ule nidhamu za darasani zilikuwa kali sana. Mwanafunzi alitakiwa kukariri karibu masomo yote, yaani unatakiwa kukumbuka mambo yote uliyojifunza, halafu kuweza kuyaeleza bila makosa wakati mwalimu alipokutaka kufanya hivyo. Katika darasa la jirani, utaona kitu kikbwa, ambacho ni kitu maalumu cha mwalimu, alikuwa anakaa juu mbele ya darasa, na wanafunzi wanatakiwa kutii amri zake."

    Prof. Ronnie Mulryne ameeleza kuwa, lugha ya Kilatini ilikuwa ni somo muhimu katika shule za enzi ya Tudor. Ingawa Shakespeare alipokuwa kijana huenda alikuwa ni sawasawa na wenzake, alichukia nidhamu kali za shuleni, lakini labda alikuwa na hamu ya kujifunza lugha ya kilatin.

    "Waandishi wa Kilatin, kama vile Ovid, huenda ni watu waliopendwa na kuheshimiwa na Shakespeare. Mashairi na opera za Shakespeare zilinukuu mara kwa mara kazi za Ovid, au Virgil na Cicero. Shakespeare aliweza kutumia vizuri kilatin, kwa hiyo kwa upande wa masomo ya lugha hii, hakika alifanya bidii."

    Ili kuwafanya watalii waweze kupata hisia za moja kwa moja, walimu na wanafunzi wa shule ya mfalme Edward VI waliigiza jinsi ilivyokuwa wakati wa somo la lugha ya kilatin enzi ya Tudor.

    Mbali na elimu ya kimsingi, kwenye ukumbi wa mji wa Stratford, kijana Shakespeare pia alipata ufahamu wa mwanzo kuhusu opera. Prof. Ronnie Mulryne ameeleza kuwa, baba ya Shakespeare, John Shakespeare aliwahi kufanya kazi katika ukumbi wa mji huo, ambao pia ulikuwa ni sehemu ya umma ya pekee iliyoweza kuonesha opera mjini Stratford.

    "Wakati Shakespeare alipokuwa kijana, opera zaidi ya 30 ziliwahi kuoneshwa kwenye ukumbi wa mji wa Stratford. Wakati huo bendi hodari za opera za mji wa London na hata Uingereza zote ziliwahi kucheza opera hapa. Tunaweza kufikiria kwamba, baada ya kutazama opera hizi, huenda aliwahi kusema 'napenda opera, na pia nitafanya kazi hii katika siku za baadaye.'"

    Sawasawa na Shakespeare aliyekuwa anapenda sana opera alipokuwa kijana, mwanafunzi wa sasa mwenye umri wa miaka 17 wa shule ya mfalme Edward VI, George Hodson pia alionesha shauku kubwa kwa opera. Anasema,

    "Tumetumia muda mwingi kwenye jengo hili la kihistoria, polepole tumeweza kufahamu jinsi Shakespeare alivyokuwa akisoma na kuishi, na kwa vipi alipata mawazo ya opera zake. Hata hivyo hatutatumia muda mwingi zaidi kujifunza na kutafiti kazi za Shakespeare kwa sababu tunasoma katika shule aliyosoma, lakini tunapojifunza na kuigiza opera zake, kweli tunaweza kupata hisia maalumu zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako