• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ahutubia mkutano wa kwanza wa utalii na maendeleo duniani

    (GMT+08:00) 2016-05-19 16:26:52

    Mkutano wa kwanza wa utalii na maendeleo duniani ulioandaliwa kwa pamoja na serikali ya China na Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Mataifa unafanyika hapa Beijing, na kuhudhuriwa na wajumbe karibu elfu moja kutoka nchi 107 duniani. Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang akihutubia mkutano huo amesema, maendeleo ya sekta ya utalii yanahitaji mazingira ya amani, na pia yanahimiza maendeleo na amani.

    Waziri mkuu Li akijulisha mchango uliotolewa na sekta ya utalii ya China kwa maendeleo endelevu ya uchumi wa China ameeleza kuwa, mwaka jana idadi ya watalii wa China waliosafiri ndani ya nchi ilifikia bilioni 4, huku mapato yaliyotokana na sekta hii yakifikia dola za kimarekani bilioni 615. Bw. Li ameongeza kuwa, sekta ya utalii imeiletea China manufaa makubwa katika kuondoa umaskini na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa.

    "Kauli mbiu ya mkutano huo "Utalii Wahimiza Maendeleo na Amani" ina maana kubwa. Ikiwa na uwazi na uvumbuzi China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali katika kusukuma mbele maendeleo endelevu na shirikishi ya sekta ya utalii, na kuhimiza kujenga aina mpya ya uhusiano wa kimataifa inayozingatia ushirikiano wa kunufaishana, ili kuleta manufaa kwa watu wa nchi mbalimbali."

    Hata hivyo Bw. Li Keqiang ametoa mapendekezo matatu kuhusu maendeleo ya sekta utalii.

    "China inapendekeza mpango wa ushirikiano wa utalii wa kimataifa utekelezwe, ili kuweka mazingira yenye urahisi zaidi, nchi mbalimbali zinatakiwa kulegeza zaidi sera zao za utoaji wa viza, kurahisisha utaratibu wa kuingia kwenye nchi zao, kuzindua safari nyingi zaidi za ndege za moja kwa moja, na kutoa huduma bora zaidi kwa ajili ya watalii, wasafiri na wateja."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako