• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pili wa UNEA wafunguliwa jijini Nairobi

    (GMT+08:00) 2016-05-24 09:16:52

    Mkutano wa pili wa Baraza la Mazingira la umoja wa Mataifa , UNEA 2 ulifunguliwa rasmi jana katika makao makuu ya Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa , UNEP, jijini Nairobi.

    Mkutano huu wa siku tano wenye kauli mbiu ya "Mazingira salama,Watu wenye Afya" umewakutanisha mawaziri na wajumbe waandamizi kutoka nchi 193 wanachama na unatarajiwa kuja na maazimio ya usimamizi wa mazingira, maendeleo endelevu na jinsi ya kukabiliana na uchafuzi wamazingira.

    Tayari wajumbe zaidi ya 2000 wakiwemo mawaziri wa mazingira, wajumbe wa serikali, na wadau mbalimbali wa mazingira wamewasili jijini Nairobi kushiriki katika mkutano huo.

    Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Mazingira wa Shirika la umoja Mataifa ,UNEP, Bw Achim Steiner amesema mkutano huo utatoa fursa ya maisha mazuri kwa kizazi kijacho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako