• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya biashara ya huduma ya kimataifa ya China inatarajiwa kufikia dola za kimarekani trilioni moja ifikapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2016-05-24 17:55:21

    Thamani ya jumla ya biashara ya huduma ya kimataifa ya China inatarajiwa kufikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni moja mpaka kufikia mwaka 2020, na kuongezeka kwa asilimia zaidi ya kumi kwa mwaka.

    Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa idara ya biashara ya huduma ya kimataifa iliyo chini ya wizara ya biashara ya China Bibi Qiu Lixin alipozungumza na waandishi wa habari kabla ya maonyesho ya biashara ya huduma ya kimataifa ya Beijing yatakayoanza Jumamosi.

    Bibi Qiu amesema, mafungamano ya kiuchumi yanaendelezwa kwa kasi duniani, hadhi ya sekta ya huduma inaendelea kuinuka katika mlolongo wa thamani wa dunia. Sekta ya huduma inavutia mitaji mingi zaidi kutoka nje ya China, na kutoa fursa mpya kwa China kupokea uhamishaji wa shughuli za huduma za kimataifa.

    Mbali na hayo, kwa mujibu wa hali ya ndani ya China, hadhi ya kimkakati ya uchumi wa huduma imeinuka wakati uchumi wa China unaingia kwenye hali mpya ya kawaida, biashara ya huduma inatoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza ongezeko la pato la taifa GDP, kupanuka kwa uwekezaji, manunuzi ya biadhaa na nafasi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako