• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Afrika wapongeza mpango wa benki ya maendeleo ya Afrika kuhimiza maendeleo

    (GMT+08:00) 2016-05-25 11:24:24

    Viongozi wa Afrika wamepongeza benki ya maendeleo ya Afrika kwa kutaja maeneo matano ya kipaumbele ya kuhimiza maendeleo ya Afrika na kuhakikisha uungaji mkono kwa benki hiyo.

    Benki hiyo imetaja maeneo matano ya kipaumbele ikitilia maanani mageuzi ya Afrika ikiwemo kutoa nishati kwa Afrika, kuunganisha Afrika, kuhakikisha chakula, kuendeleza viwanda na kuboresha maisha ya waafrika.

    Maeneo hayo matano ya kipaumbele yaliwekwa katika mkakati wa miaka 10 ya benki hiyo na kuwa kama mwongozo kwa nchi za Afrika kufanya mageuzi endelevu.

    Rais Idriss Deby Itno wa Chad ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, amesema mkakati wa benki hiyo kwa maendeleo ya Afrika utasaidia ongezeko la uchumi la bara la Afrika. Ameongeza kuwa viongozi wa Afrika watahakikisha benki hiyo inatekeleza ahadi zote kuwa manufaa halisi kwa waafrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako