• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia atangaza kugombea nafasi ya mkurugenzi mkuu wa WHO

    (GMT+08:00) 2016-05-25 15:33:27
    Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus ametangaza rasmi kuwa atagombea nafasi ya mkurugenzi mkuu ajaye wa Shirika la Afya Duniani WHO.

    Akizungumza na waandishi wa habari kando ya kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Afya Duniani kinachofanyika Geneva, Bw. Ghebreyesus amesema akishinda wadhifa huo, ataliongoza Shirika la Afya Duniani WHO kutoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa, huduma za kimsingi za afya zinafikia kila mtu, kuzidisha uwezo wa Shirika hilo wa kukabiliana na matukio ya dharura, na kuboresha hali ya afya na tiba kwa wanawake na watoto.

    Bw. Ghebreyesus ambaye ni mtaalamu maarufu wa kimataifa katika utafiti wa ugonjwa wa malaria, alikuwa waziri wa afya wa Ethiopia tangu mwaka 2005 hadi 2012, na ni mgombea pekee barani Afrika aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika mwezi Januari mwaka huu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako