• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuunga mkono Umoja wa Afrika kuimarisha uwezo wa pamoja wa kulinda usalama

    (GMT+08:00) 2016-05-25 16:34:11

    Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi ametoa mwito kwa Umoja huo kuunga mkono zaidi Umoja wa Afrika kuimarisha uwezo wa pamoja wa kulinda usalama barani Afrika.

    Akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana kuhusu ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika masuala ya amani na usalama, Balozi Liu amesema, China inatumai Umoja wa Mataifa utatoa msaada zaidi kwa ajili ya suala hilo, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo na ufadhili zaidi, kuunga mkono wanajeshi wa kuchukua hatua wanapohitajika wa Afrika na vikosi vya kukabiliana na matukio ya dharura vya Afrika, ili kupambana na ugaidi barani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako