• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kambi inayomuunga mkono rais wa DRC kuandaa maandamano ya amani nchini humo

    (GMT+08:00) 2016-05-25 18:14:14

    Idara ya siasa ya upande unaomuunga mkono rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imetangaza kuwa itaandaa maandamano ya amani ya siku mbili nchini humo kuanzia hii leo.

    Waandaaji hao wamesema, maandamano hayo yanalenga kuonyesha kumuunga mkono rais Joseph Kabila kufuatia uamuzi uliotolewa hivi karibuni na Mahakama ya Katiba nchini humo unaomruhusu rais huyo kuendelea kuongoza nchi mpaka uchaguzi mkuu utakapofanyika.

    Maandamano hayo yanafanyika kabla ya maandamano ya upande wa upinzani yaliyopangwa kufanyika ijumaa wiki hii kupinga uamuzi huo wa mahakama.

    Mvutano wa kisiasa umeongezeka nchini DRC kutokana na uwezekano wa kuahirisha uchaguzi wa rais ambao ulipangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako