• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatetea msimamo wake kuhusu Bahari ya Kusini ya China

    (GMT+08:00) 2016-05-25 19:54:45

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying ametetea msimamo wa China kuhusu Bahari ya Kusini ya China, na kupinga ukosoaji unaofanywa na Marekani, Japan na vyombo vya habari vya Magharibi.

    Bi. Hua amesema, ujenzi unaofanywa na China kwenye vidiwa na miamba ulioanza mwishoni mwa mwaka 2013 unalenga kulinda mamlaka na haki yake.

    Kauli ya Bi. Hua imekuja baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kusema vitendo vya China kwenye Bahari ya Kusini na Mashariki ya China vinalenga kuleta mvutano. Hata hivyo, Bi. Hua amesema ni ukuaji wa vitendo vya kijeshi kwenye kanda hiyo ndivyo vinavyosababisha mvutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako