Kundi la Taliban la Afghanistan limethibitisha kifo cha kiongozi wake, Mullah Mohammad Akhtar Mansoor, kilichotokea katika shambulizi la anga mwishoni mwa wiki iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na kundi hilo kwenye mtandao wa internet imesema, kundi hilo limemteua Moulavi Haibatullah Akhundzada kuwa kiongozi mpya kushika nafasi ya Mansoor. Taarifa hiyo imesema, wajumbe wote wa kamati ya uongozi ya Taliban wameunga mkono uteuzi wa Akhundzada, ambaye alikuwa naibu wa pili wa Mansoor.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |