• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Hangzhou wajiandaa kwa ajili ya mkutano ujao wa G20

    (GMT+08:00) 2016-05-26 16:32:23
    Mji wa Hangzhou ulioko mashariki mwa China unajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa G20 utakaofanyika baadaye mwaka huu.

    Viongozi wa nchi za G20 wakiwemo rais Xi Jinping wa China na rais Barack Obama wa Marekani watahudhuria mkutano huo unaopangwa kufanyika Septemba 4 na 5.

    Meya wa Hangzhou Zhang Hongming amesema mji huo unafanya kila linalowezekana kujiandaa kwa ajili ya mkutano huo.

    Amesema, "Tangu mwaka jana tumeanza kuimarisha miundombinu, ikiwemo kujenga Subway na barabara za kasi. Tumefanya juhudi kubwa katika kuboresha mazingira katika maeneo makuu. Hususan, tunaendelea na ujenzi wa mtandao wa barabara za kasi zinazounganisha mji huu na wilaya jirani. Tunatarajia itakapofika mwishoni mwa Juni, sura ya mji huu itabadilika."

    Kauli hiyo inakuja wakati zimebaki siku 100 kabla ya mkutano huo. Mpaka sasa watu elfu 6 wamejiandikisha kutoa huduma wakati wa mkutano.

    Meya Zhang amesema mji huo unataka kutumia fursa hii kubadilika na kuwa mji wa uvumbuzi.

    Amesema, "Mwaka jana, idadi ya kampuni zilizoanzishwa imeongezeka kwa asilimia 17, huku mitaji iliyoandikishwa ikiongezeka kwa zaidi ya asilimia 56. Kwa miaka 11 mfululizo, mji wa Hangzhou umeongoza miji mingine mikuu ya mikoa mbalimbali katika upande wa uvumbuzi, ambapo mwaka jana hakimiliki za uvumbuzi ziliongezeka kwa karibu asilimia 50."

    Makao makuu ya kampuni kubwa ya Alibaba inayofanya biashara kupitia mtandao wa Internet yako mjini Hanghou, ambako kuna wakazi karibu milioni 9. Mji huo unaendela kuibuka kama kituo cha biashara kupitia mtandao wa Internet na kuwa mwenyeji wa eneo la kielelezo la kwanza nchini China la biashara ya aina hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako