• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi asema masuala ya maendeleo yatapewa kipaumbele kwenye mkutano wa G20

    (GMT+08:00) 2016-05-26 20:08:29
    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema masuala ya maendeleo yatapewa kipaumbele kwenye mkutano wa wakuu wa G20 utakaofanyika Septemba nchini China.

    Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari, Wang Yi amesema masuala hayo ambayo ni pamoja na kuzisaidia nchi zinazoendelea kuondokana na umaskini na kutimiza maendeleo, ni wajibu wa pamoja wa jumuiya ya kimataifa na yanaweza kuwa injini ya maendeleo ya uchumi wa dunia. Amesema namna ya kuvumbua njia ya maendeleo itakuwa ajenda kuu ya mkutano huo.

    Aidha, Wang amesema, matunda muhimu yanayotarajiwa kwenye mkutano huo ni pamoja na kuweka mpango wa maendeleo endelevu mwaka 2030, kuthibitisha maeneo yanayopewa kipaumbela ya kufanyiwa mageuzi, kuweka mikakati ya kuongeza biashara duniani, kuweka mwongozo wa uwekeaji duniani, na kuimarisha ushirikiano wa kupambana na ufisadi.  

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako