• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko tayari kuendesha mkutano wa kilele wa kundi la G20

    (GMT+08:00) 2016-05-27 09:05:30

    Ikiwa zimebaki siku 100 kabla ya mkutano wa kilele wa kundi la G20 utakaofanyika tarehe 4 hadi tarehe 5 Septemba huko Hangzhou, kusini mashariki mwa China, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China inakaribia kukamilisha maandalizi ya mkutano huo. Anasema,

    "Miezi sita imepita kwa mafanikio tangu China ichukue uenyekiti wa kundi la nchi 20. Ajenda zilizotolewa na China zimeungwa mkono na pande mbalimbali. Mipango ya shughuli mbalimbali za mkutano huo imethibitishwa, na ujenzi wa majumba ya mkutano umekamilika. Napenda kuwaarifu kuwa China iko tayari, na Hangzhou iko tayari. "

    Kwa sasa, uchumi wa dunia uko katika kipindi cha mageuzi, na unakua taratibu bila kuondokana na shinikizo kubwa la kupungua. Bw. Wang Yi amesema, China ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu wa kundi la G20, inapenda kufanya kazi kubwa zaidi kwa ajili ya ufufuaji wa uchumi wa dunia.

    "kupitia mkutano wa kundi la nchi 20 utakaofanyika huko Hangzhou, tutashirikiana na wadau wengine kufuatilia changamoto kuu na masuala makubwa yanayoukabili uchumi wa dunia, na kutafuta suluhisho kwa kutumia busara za China. Hatua za muda mfupi zinasaidia kurudisha ongezeko tulivu la uchumi, lakini hatua za muda mrefu zinaleta suluhisho la kudumu kwa ongezeko la muda mrefu. Tunatumai kufanya kundi la nchi 20 kubadilika kutoka utaratibu wa kukabiliana na dharura, na kuwa wa kuhimza ongezeko la muda mrefu, ili kuleta ongezeko la uchumi wa dunia na kuongoza mwelekeo wa uchumi wa kimataifa. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako