• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marcus Rashford ajiunga rasmi na kikosi cha Uingereza

    (GMT+08:00) 2016-06-01 09:15:09
    Kocha Roy Hodgson ametaja kikosi chake cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Uingereza huku mchezaji kijana wa Manchester United, Marcus Rashford, akijumuishwa rasmi katika kikosi hicho kitakachocheza michuano ya Mabingwa wa Ulaya, Euro 2016.

    Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 18, alifunga goli lake la kwanza akiichezea timu ya taifa Uingereza kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki walioshinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Australia siku ya Ijumaa.

    Mshambuliaji wa timu ya Liverpool Daniel Sturridge ameorodheshwa kwenye kikosi hicho, hata hivyo mchezaji wa Newcastle United Andros Townsend na Danny Drinkwater wa Leicester City wameachwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako