• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Twiga stars yajiandaa kwa mechi na Rwanda

    (GMT+08:00) 2016-06-01 09:16:05
    Kikosi cha Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars nchini Tanzania kinatarajia kuingia kambini hivi karibuni kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Rwanda.

    Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Alfredy Lucas, amesema timu ya Taifa ya Rwanda iliomba mchezo huo ikiwa ni katika maandalizi ya kusonga mbele katika kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake.

    Na wakati huo huo nacho kikosi cha Timu ya Taifa ya Misri kinatarajiwa kuwasili leo nchini Tanzania kwa ajili ya mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars wa kuwania fainali za AFCON utakaopigwa jumamosi ya Juni 04 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Misri hapo mwaka jana, Taifa Stars ilipoteza mchezo huo baada ya kuchapwa mabao 3-0.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako