• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Infantino apinga pendekezo la kupunguziwa mshahara

    (GMT+08:00) 2016-06-01 09:16:33
    Rais wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA), Gianni Infantino amekataa pendekezo linalotaka mshahara wake kupunguzwa akisema kiasi kinachopendekezwa na kamati ya mishahara ni 'matusi'.

    Kulingana na gazeti la Chicago Tribune, kamati hiyo imependekeza Infantino aliyejaza nafasi Sepp Blatter kulipwa takriban dola laki mbili kila mwaka.

    Mshahara huu ni dola laki moja chini ya ule Blatter alikuwa anapokea.

    Infantino mwenye umri wa miaka, 45, alikataa pendekezo la kukatwa mshahara kabla ya kongamano ya wanachama 211 wa FIFA lilofanyika jijini Mexico City.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako