• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashabiki wamtaka kocha wa Harambee Stars aanze kushinda mechi.

    (GMT+08:00) 2016-06-01 09:17:02
    Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Stanley Okumbi amekiri anakabiliwa na presha kali kutoka kwa mashabiki wanaomtaka aanze kushinda mechi.

    Akizungumza baada ya kuongoza Kenya kuandikisha sare ya pili mfululizo ilipokabwa 1-1 na Sudan, Okumbi alisema Jumanne kuwa kushinda Congo Brazzaville mnamo Juni 3 siyo muhimu tu kwa taifa, bali pia kwake binafsi.

    Okumbi aliwaacha nje wachezaji kama nahodha Victor Wanyama anayechezea klabu ya Southampton, Uingereza, Ayub Timbe anayesakata kwenye klabu ya Lierse, Ubelgiji, David Owino na Anthony Akumu na hata kipa Boniface Oluoch, miongoni mwa wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako