• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabondia walaani uamuzi wa AIBA kuruhusu mabondia wa kulipwa kwenye Olimpiki ya Rio

    (GMT+08:00) 2016-06-02 09:59:33
    Bingwa wa zamani wa dunia wa masumbwi Carl Frampton na mabondia wengine mbalimbali wamekosoa uamuzi wa kuruhusu mabondia wa kulipwa kupigana kwenye michezo ya olimpiki. Jumatano hii chama cha ndondi cha kimataifa, AIBA kilikubali kubadilisha sheria inayowazuia mabondia hao kabla ya michezo hiyo inayoanza Agosti 5. Chama cha ndondi cha Uingereza kimeitaka AIBA kufikiria zaidi uamuzi wake wakisema ni wa hatari. Kimesema ni kinyume na moyo wa Olimpiki, na ni kutowaheshimu mabondia wengi ambao si wa kulipwa wa Uingereza. Wamesema kuwapiganisha mabondia wa kulipwa na wasiolipwa ni wazimu. Mabondia wa kulipwa akiwemo Floyd Mayweather wanaweza kushiriki kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu na kuwania medali kwa mara ya kwanza. Jumla ya mabondia 286 watashiriki kwenye mashindano hayo. Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Mike Tyson, aliyewahi kushinda medali ya dhahabu kipindi anacheza ngumi za ridhaa mwaka 1981 na 1982 kwenye Junior Olympic Games, naye pia ameikosoa hatua hiyo. Mabondia waliowahi kushiriki mashindano hayo kabla ya kuingia kwenye ndondi za kulipwa ni pamoja na Muhammad Ali, Joe Frazier, George Foreman, Lennox Lewis, Oscar De La Hoya na Vladimir Klitschko.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako