• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri kumenyana na Taifa Stars Jumamosi hii

    (GMT+08:00) 2016-06-02 10:01:17
    Kikosi cha Timu ya Taifa ya Misri kinatarajiwa kumenyana na Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars katika mechi za kuwania fainali za AFCON siku ya jumamosi ya Juni 04 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF, Alfredy Lucas amesema, mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Gabon huku taratibu zote kuhusu mchezo huo zikiwa zimekamilika. Katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Misri hapo mwaka jana, Taifa Stars ilipoteza mchezo huo baada ya kuchapwa mabao 3-0. Baada ya mchezo dhidi ya Misri, Stars itacheza mechi ya mwisho na Nigeria Mjini Lagos Septemba mwaka huu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako