• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijidudu viliwahi kula nusu ya hewa duniani

    (GMT+08:00) 2016-06-03 14:54:25

    Viumbe vikilinganishwa na dunia yetu ni vidogo sana, ambavyo ni kama vumbi linalofunika ardhini. Maisha yao yanayoweza kudumu kwa siku kadhaa hadi miaka mia kadhaa pia ni mafupi sana yakilinganishwa na historia ya dunia yetu ambayo ni miaka bilioni 4.6. Lakini unaamini kuwa vijidudu vidogo sana viliwahi kula nusu ya hewa dunia?

    Mwezi uliopita Dr. Sanjoy Som wa Chuo Kikuu cha Washington alitoa makala kwenye gazeti la Nature Geoscience akisema utafiti unaonesha kwamba katika miaka bilioni 3 iliyopita kiasi cha hewa duniani kilikuwa chini ya nusu ya cha siku hizi.

    Kama tunavyojua, Oxygen inachukua moja ya tano tu ya hewa zote, hivyo bila shaka mabadiliko makubwa kama hayo yalisababishwa na hewa ya Nitrogen ambayo ni nyingi zaidi. Katika kipindi cha Archean (miaka bilioni 4 hadi bilioni 2.5 iliyopita), vijidudu vilianza kuishi duniani. Chakula cha vijidudu hivi kilikuwa cha ajabu, vilivuta hewa ya Nitrogen moja kwa moja ili kuzalisha asidi amino ambayo ni lishe muhimu kwa viumbe vingi. Baada ya asidi amino kutumiwa na vijidudu hivi, ikawa vigumu kubadilika tena kuwa hewa ya Nitrogen, ililibadilika kuwa Ammonia na kulimbikizwa ardhini.

    Ilipofika kipindi cha Proterozoic (miaka bilioni 2.5 hadi milioni 542 iliyopita), vijidudu vinavyofanya usanisinuru vilianza kuishi duniani, na kutoa hewa nyingi ya Oxygen. Hewa hiyo inaweza kufanya vitu mbalimbali viwe na oksijeni vikiwemo mawe na udogo, na kusababisha Nitrogen inayolimbikizwa ardhini kurudishwa hewani. Hayo ndiyo mabadiliko ya hewa katika historia ndefu ya dunia yetu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako