• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Mei - 3 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-03 16:36:30

    Aliyekuwa Rais wa Chad Hissene Habre afungwa miaka 20

    Aliyekuwa Rais wa Chad Hissene Habre amepatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuamrisha kuteswa na kuuwawa kwa maelfu ya wapinzani wake wa kisiasa wakati wa utawala wake wa miaka 8 ulioanza 1982.

    Alihukumiwa kifungo cha maisha na kitengo maalum cha Umoja wa Afrika kilichoundwa mwaka wa 2-13 na Senegal na Umoja huo.

    Kesi yake imeamuliwa baada ya waathiriwa na wanaharakati wa kutetea haki kusubiri kwa miaka 16.

    Hissene alitoroka nchini Chad baada ya kupinduliwa mwaka wa 1990.

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Ban Ki Moon amesema hukumu ya Bw Hissene Habre ni alama ya kihistoria katika sheria za kimataifa.

    Bw Ban Ki Moon ameupongeza Umoja wa Afrika na hasa Senegal kwa kuanzisha mahakama maalum, na amezishukuru nchi zote zilizochangia kufanikishwa kwa hukumu hiyo.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako