• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Mei - 3 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-03 16:36:30

    Kundi la waasi la M23 la DRC lakubaliwa kuwa chama cha siasa

    Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imelikubalia rasmi kundi la zamani la waasi M23 liwe chama cha siasa, na kuitwa Muungano wa Kuwakomboa Watu ASP.

    Usajili wa chama hicho umethibitishwa kupitia amri ya waziri wa mambo ya ndani Evariste Boshab iliyosainiwa Jumatatu wiki hii.

    Kiongozi wa chama hicho Jean-Marie Runiga amesema, chama hicho kitaendelea kuwepo katika utaratibu wa muda wa mpito wa rais Joseph Kabila.

    Mmoja wa waanzilishi wa chama hicho Moise Tshokwe amesema, chama hicho kinataka kitambuliwe kama cha kiraia katika mazungumzo yote na serikali.

    Kundi la waasi la M23 lilianzishwa baada ya vita kutokea mashariki mwa DRC mwezi April mwaka 2012.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako