• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (30 Mei - 3 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-03 16:36:30

    Sudan yakataa kujiunga na kamati ya kikanda ya kupambana na kundi la LRA

    Serikali ya Sudan imekataa kujiunga na kamati ya kikanda ya kupambana na kundi la waasi la Uganda la Lords resistance Army, ikisema kuwa kundi hilo halipo kwenye ardhi ya kikanda.

    Gazeti la Tribune la Sudan limenukuu ofisa mwandamizi wa Sudan akisema Sudan imekataa pendekezo kujuinga na kamati hiyo, baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkutano wa tano wa mawaziri wa juhudi za kikanda za kulitokomeza kundi la Lords resistance army.

    Ofisa huyo wa Sudan amesema kwa sasa hakuna uhusiano kati ya Sudan na kundi la LRA, hasa baada ya Sudan kutendana na Sudan kusini, na kutokuwa na mpaka na Uganda.

    Habari za hivi karibuni zilitaja kuwa kiongozi wa kundi la LRA Bw Joseph Kony alikuwa kwenye eneo la Kafia Kanji, eneo la mpakani linalogombewa kati ya Sudan na Sudan Kusini. Mwezi Septemba maofisa wa Umoja wa Afrika walikwenda Sudan kujadili suala hilo na maofisa wa serikali na jeshi, lakini walikana kuwa Sudan inawahifadhi wapiganaji wa LRA.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako