• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Unajua nguo unazovaa kama zinachafua mazingira na hata nyuzi zinaingia mwilini?

    (GMT+08:00) 2016-06-03 15:04:30

    Ripoti iliyotolewa kwenye mkutano wa pili wa mazingira wa Umoja wa Mataifa uliofanyika hivi karibuni mjini Nairobi inaonesha kuwa nguo zilizotengenezwa kwa nyuzi za kemikali zikifuliwa katika mashine za kufulia nguo, msuguano unasababisha vipande vidogovidogo vya nyuzi hizi viingine majini. Nguo moja inaweza kutoa vipande zaidi ya 1900 kila mara inapofuliwa. Vipande hivi ni vidogo sana haviwezi kuchujwa na vifaa vya kusafisha maji, na mwishowe huingia mwilini mwa binadamu kwa njia mbalimbali.

    Ukaguzi kuhusu samaki wa baharini waliouzwa katika masoko ya Indonesia na jimbo la California nchini Marekani unaonesha kuwa, robo moja ya viungo vya ndani vya samaki vina viwembe vya plastiki na vipande vya nyuzi za nguo. Licha ya samaki, wakaguzi pia wamegundua viwembe vidogo vya plastiki kwenye maji ya kunywa, bia, asali, sukari na chumvi.

    Maisha ya binadamu pia yamesababisha uchafuzi wa mazingira kwa njia nyingine mbalimbali. Miji ya duniani inatoa tani bilioni 7 hadi bilioni 10 za takataka kila mwaka. Takataka zikichomwa zinatoa hewa yenye sumu, na zikizikwa kwa njia isiyo sahihi, zinachafua maji chini ya ardhi.

    Ripoti ya Umoja wa Mataifa pia inaonesha kuwa magari ni sababu kuu ya uchafuzi wa hewa. Katika nchi za Ulaya, asilimia 30 ya vumbi linasababishwa na magari, na uchafuzi wa hewa uliotokana na magari umeleta hasara ya dola za kimarekani bilioni 137 kwa mwaka.

    Umoja wa Mataifa unasema, hadi pale mazingira yatakapoboreshwa hatua kwa hatua, binadamu ndio wataweza kudumisha furaha yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako