• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijidudu vinavyoweza kubadilisha rutuba kuwa nishati

    (GMT+08:00) 2016-06-03 15:05:32

    Chuo Kikuu cha Hiroshima na Taasisi ya utafiti wa mwamba chini ya ardhi ya Horonobe nchini Japan wamegundua kuwa vijidudu aina ya Clostridium vinaweza kuozesha rutuba zilizoko chini ya ardhi, vikifanya kazi pamoja na vijidudu aina ya Methanogenus, vinaweza kuzalisha hewa ya Methane ambayo inaweza kuchomwa na ni nishati nzuri.

    Viumbe vikifa vinabadilika na kuwa rutuba. Rutuba hizi zimelimbikiza asilimia 10 kati ya Carbon zote zilizoko kwenye gamba la dunia, na zimechukuliwa kuwa chanzo cha makaa ya mawe. Rutuba hizi zikioza zaidi huenda zikatoa hewa ya Methane, lakini zamani wanasayansi hawakugundua njia ya kubadilisha rutuba hizi kuwa nishati.

    Kikundi cha utafiti cha Chuo Kikuu cha Hiroshima kilipokea vijidudu aina ya Clostridium vilivyokusanywa chini ya ardhi katika mazingira yasiyo na hewa ya Oxygen, na kugundua kuwa vijidudu hivi vinaweza kuozesha rutuba, na vitu vinavyotokea baada ya kuoza ni chakula cha vijidudu aina ya Methanogenus, ambavyo vinaweza kuzalisha hewa ya Methane bila ya hewa ya Oxygen.

    Kikundi hiki kinapanga kulea vijidudu vya aina mbili kwa pamoja ili kuthibitisha kama vinaweza kuzalisha hewa ya Methane au la.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako