• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sababu 5 kuu za ajali za ndege

    (GMT+08:00) 2016-06-03 15:05:48

    Habari yoyote ya ajali ya ndege inawasababisha watu wengi wawe na wasiwasi kuhusu usalama wa ndege, na kushuku kama kuna mashambulizi ya kigaidi au la. Lakini ukweli ni kwamba kuna sababu mbalimbali na makosa ya rubani ndio sababu kuu zaidi.

    1. Makosa ya rubani

    Siku hizi ndege zina sifa nzuri zaidi na zinaaminika zaidi, hivyo makosa ya rubani yamesababisha ajali nyingi za ndege, ambazo zinachukua asilimia 50 ya ajali zote. Ndege ni chombo chenye utatanishi mkubwa. Rubani wanapoendesha ndege kwa hatua mbalimbali, ni rahisi kufanya makosa.

    2. matatizo ya vifaa kwenye ndege

    Ingawa ndege zinasanifiwa na kutengenezwa vizuri zaidi siku hadi siku, lakini asilimia 20 ya ajali za ndege bado zinasababishwa na matatizo ya vifaa kwenye ndege. Injini ikishindwa kufanya kazi, ajali zitatokea.

    3. Hali mbaya ya hewa

    Asilimia 10 ya ajali za ndege zinasababishwa na hali mbaya ya hewa. Ingawa vifaa vingi vipya vya elektroniki vimewekwa kwenye ndege, vikiwemo gurudumu tuzi, GPS na mfumo wa data za hali ya hewa, lakini ndege bado ni dhaifu zikikabiliwa na dhoruba, theluji kubwa na ukungu.

    4. Vitendo vya kuharibu ndege kwa makusudi

    Asilimia 10 ya ajali za ndege zinasababishwa na vitendo vya kuharibu ndege kwa makusudi. Lakini ni kweli njama hizi zimesababisha ajali nyingi na hasara kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako