• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hofu ya wazazi inaweza kuhisiwa na watoto wachanga?

    (GMT+08:00) 2016-06-03 15:06:07

    Watafiti waligundua kuwa panya jike mwenye hofu anaweza kuwafanya watoto wake wachanga wawe na hofu kupitia harufu yake.

    Watafiti walifanya majaribio ya kuumiza miguu ya baadhi ya panya jike kwa umeme wakati wanapohisi harufu ya nanaa ili kuwafanya kuogopa harufu hiyo. Baada ya panya hao kuzaa watoto, baadhi ya panya jike waliendelea kuhisi harufu ya nanaa wakati walipoumizwa, na wengine hawakufanyiwa hatua hizi. Kundi lingine la panya jike lilihisi harufu ya nanaa lakini hawajawahi kuumizwa miguuni. Matokeo ya majaribio yanaonesha kuwa watoto wa panya jike wa kundi la kwanza waliogopa zaidi harufu ya nanaa. Hofu hiyo iliendelea mpaka umri wa siku 43 ambapo waliingia kipindi cha ujana. Hii inamaanisha kuwa baada ya kuhisi kemikali fulani inayotolewa na mama zao, panya wadogo wanashikwa na hofu. Baada ya kukagua bongo zao, watafiti wamegundua kuwa sehemu ya Amygdala ya bongo zao ndiyo sehemu inayowahimiza wawe na hofu. Uwezo wa kuhisi hofu ya wazazi unawasaidia panya wadogo kutofautisha hali ya hatari na salama. Na wanyama wengine wengi pia wana uwezo huo. Lakini pia huenda ukawasababisha watoto kusumbuliwa na tatizo la kuwa na hofu kupita kiasi. Kwa mfano, ni rahisi kwa mtoto mchanga aliyezaliwa na mama mwenye unyogovu kukumbwa na matatizo mbalimbali ya hisia, ukiwemo wasiwasi wa kutengwa na mama yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako