• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tunaweza kuwaokoa vifaru weupe wa kaskazini kwa teknolojia ya biolojia?

    (GMT+08:00) 2016-06-03 15:06:52

    Vifaru weupe wa kaskazini wanakaribia kutoweka. Kutokana na uwindaji haramu, idadi ya vifaru hawa imepungua na kubaki watatu tu kutoka 2300. Sasa vifaru hao watatu wanaishi katika hifadhi ya Ol Pejeta nchini Kenya, na kulindwa kwa makini na walinzi wenye bunduki siku nzima. Lakini hatua hiyo haisaidii kuzuia kutoweka kwao, kwa sababu kifaru pekee dume aitwaye Sudan ana umri wa miaka 43 na ni mzee sana. Mtoto wake jike aitwaye Najin aliwahi kujeruhiwa miguuni, hafai kuwa na mimba. Mtoto wa Najin aitwaye Fatu ana tatizo la uzazi. Licha ya matatizo hayo, wote wanatoka familia moja, hawafai kuzaliana.

    Hivi karibuni watafiti wa bustani ya wanyama ya San Diego na taasisi ya Leibniz ya Ujerumani wametoa mpango kwenye gazeti la biolojia ya wanyama, wakisema mbegu za kiume na seli za vifaru kumi waliokufa zinahifadhiwa katika maabara mbalimbali duniani, wanapanga kutumia teknolojia saidizi za uzazi kukuza mimba na kuiweka kwenye tumbo la kifaru jike mweupe wa kusini ili asaidie kuzaa mtoto.

    Maendeleo ya teknolojia ya biolojia huenda yataweza kuwasaidia wanyama wenye matatizo ya uzazi kuzaa tena, lakini teknolojia haiwezi kutimiza malengo yote. Tukifanikiwa kuwasaidia vifaru hao kuzaa tena, bado watakuwa tofauti na vifaru pori wa zamani. Kwa sababu wanyamapori wana jeni tofauti, kutokana na uteuzi wa kimaumbile, wanabadilika ili kuendana na mazingira. Lakini wale waliozaliwa kwa teknolojia ya biolojia wana jeni zinazofanana, hawawezi kubadilika katika uteuzi wa kimaumbile.

    Mustakabali wa mpango wa kuwaokoa vifaru weupe wa kaskazini bado haujajulikana. Ni muhimu zaidi kuwahifadhi wanyama wengine ili wasikabiliwe na hali ya kusikitisha ya kutoweka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako