• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Stanley Okumbi aabdikisha ushindi wa kwanza

    (GMT+08:00) 2016-06-06 09:49:02

    Kocha wa timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars Stanley Okumbi ni mwingi wa furaha baada ya kuonja ushindi wake wa kwanza kama kocha mkuu wa Kenya inayokamata nafasi ya 129 duniani alipoiongoza kupiga nambari 60 Congo Brazzaville 2-1 uwanjani Kasarani.

    Okumbi ambaye alipoteza mechi zake mbili za kwanza dhidi ya Guinea-Bissau mwezi Machi zilizozima kabisa matumaini ya Kenya kufuzu kushiriki Kombe la Afrika mwaka 2017, alikiri Kenya inahitaji mechi nyingi za kirafiki kabla ya mechi muhimu.

    Awali Kenya ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Tanzania na tena ikaandikisha matokeo sawa na hayo dhidi ya Sudan uwanjani Kasarani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako