• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyangumi wauaji wana tamaduni tofauti, ambazo hata zinaathiri mabadiliko ya jeni zao

    (GMT+08:00) 2016-06-07 14:41:43

    Jeni za binadamu zinabadilika kufuatia tamaduni zao. Mfano mzuri ni kwamba baada ya kushughulikia kilimo na ufugaji katika muda mrefu uliopita, baadhi ya binadamu wamepata uwezo wa kumeng'enya laktosi kwenye maziwa. Watafiti wengi wanaamini kuwa tamaduni zimehimiza mabadiliko ya binadamu. Na ushahidi umethibitisha kuwa tamaduni tofauti pia zimehimiza mabadiliko ya nyangumi wauaji.

    Nyangumi wauaji wanaishi katika makundi na mazingira mbalimbali na wanawinda kwa njia za kipekee. Kwa mfano, baadhi ya nyangumi wanajifanya kama wamekwama ufukweni ili kuwashawishi sili kuwakaribia. Baadhi yao wanashirikiana kuwafanya samaki kukusanyika pamoja na kuwasaka samaki hao kwa urahisi. Jambo la kushangaza ni kwamba njia hizi za uwindaji zinarithiwa kizazi baada ya kizazi. Nyangumi hao huishi katika makundi yao kwa miongo kadhaa, hivyo watoto wao wana fursa nyingi za kujifunza namna ya kuwinda. Wanabiolojia wameeleza vitendo hivi kwa neno la "tamaduni".

    Lakini sawali ni kwamba je makundi ya nyangumi wauaji yenye tamaduni tofauti yana jeni tofauti au la? Dr. Andrew Foote kutoka Chuo Kikuu cha Bern cha Uswisi na wenzi wake wametafiti jeni za nyangumi 50 kutoka makundi matano, na kugundua kuwa jeni zao pia ni za aina tano, ambazo zinaendana na makundi yao. Ingawa nyangumi wauaji wana mababu sawasawa katika miaka laki 2 iliyopita, lakini ni wazi kwamba jeni zao zimebadilika kufuatia tamaduni zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako