• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chimbuko la mbwa liko wapi?

    (GMT+08:00) 2016-06-07 14:42:30

    Katika miaka mingi iliyopita wanasayansi wamekuwa wakijadiliana sana kuhusu chimbuko la mbwa. Baadhi yao wanasema liko China au Mashariki ya Kati, na baadhi yao wanasema liko Ulaya. Utafiti mpya unasema maoni hayo huenda yote ni sawa.

    Utafiti uliotolewa hivi karibuni katika gazeti la Sayansi la Marekani unasema baada ya kufugwa na binadamu, mbwa mwitu walibadilika na kuwa mbwa, mara mbili. Mara moja ilitokea huko Ulaya na mara nyingine ilitokea Asia.

    Watafiti wametafiti jeni za mbwa wa Ireland aliyeishi katika miaka 4,800 iliyopita, na DNA za mbwa wengine 59 walioishi huko Ulaya katika miaka elfu 14 hadi elfu 3 iliyopita. Wamezilinganisha jeni hizi na jeni za mbwa 685 wa aina mbalimbali za kisasa, na kugundua kuwa mbwa mwitu wote walibadilika kuwa mbwa baada ya kufugwa na binadamu huko Ulaya na Asia, lakini katika miaka elfu 14 hadi elfu 6 iliyopita, mbwa waliofugwa huko Asia walihamia Ulaya wakiwafuata binadamu. Baada ya kuzaliana na mbwa wenyeji wa Ulaya, jeni za mbwa wa Asia zilichukua nafasi ya zile za mbwa wa Ulaya.

    Prof. Greger Larson wa Chuo Kikuu cha Oxford amesisitiza kuwa, utafiti huo ni nadharia tu, bado wanahitaji kutafuta ushahidi wa aina nyingi zaidi ili kuuthibitisha. Lakini kwa mujibu wa jeni za mbwa wa kale na rekodi za akiolojia, watu wanatakiwa kufikiria uwezekano kwamba watu wa kale wa Ulaya na Asia wote waliwafuga mbwa mwitu na kuwabadilisha kuwa mbwa wa kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako