• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waendesha mashtaka Wataka Neymar ashtakiwe kwa udanganyifu

    (GMT+08:00) 2016-06-08 09:23:33

    Waendesha mashtaka wamemtaka nyota wa Brazil na Barcelona Neymar kushtakiwa kwa udanganyifu wa fedha.

    Waendesha mashtaka hao kutoka mahakama ya kukabiliana na uhalifu nchini Uhispania wanadai kwamba Neymar na babaake walificha thamani ya uhamisho wa mchezaji huyo kutoka Santos hadi Barcelona

    Katika mahojiano ya awali Neymar amekana kufanya makosa yoyote.

    Hazina moja ya uwekezaji ambayo ilimiliki asilimia 40 ya haki za Neymar indai kwamba haikupata mgao wake kamili.

    Barcelona inasema kwamba ililipa Yuro milioni 57 kumnunua Neymar mwaka 2013 huku wazazi wake Neymar da Silva Santos na Nadine Goncalves da Silva Santos akipata wakipokea Yuro milioni 40 na kilabu yake ya zamani Santos ikipokea Yuro milioni 17.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako