• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zingatia afya ya macho yako!

  (GMT+08:00) 2016-06-08 14:04:05

  Siku hizi, kutokana na kusambaa kwa simu na kompyuta, inaonekana kama watu hawawezi kuishi bila kutumia vitu hivi. Katika hali hiyo, tunatumia macho yetu kupita kiasi, kwa hiyo, lazima tuzingatie afya ya macho yetu. Na unapokuwa na dalili zifuatazo za macho, inafaa uchukue tahadhari:

  1. Huwezi kuona vizurii kitu au huwezi kuona chochote kwa muda mfupi tu, lakini baadaye unarejea kwenye hali yako ya kawaida;

  2. Ukitazama vitu, unahisi kama vitu vinapinduka au vimebadilika rangi na kuwa nyekundu au manjano;

  3. Kama ukihisi kuna kivuli cheusi kidogo cha doa ukitazama kitu

  4. Na ukisikia maumivu ya macho mara kwa mara, lazima uende kwa daktari ukaangaliwe macho yako.

  Na hadi hapo, watu wengi hupendelea kujua, tutafanyaje ili kuepuka kuharibu macho yetu kadiri tuwezavyo?

  1. Usitazame screen ya kompyuta kwa muda mrefu sana, ni vyema uchukuae muda wa kupumzika kwa dakika 5-10, kila baada ya kufanya kazi kwa kutumia kompyuta kwa saa moja;

  2. Kaa vizuri na tazama screen kwa umbali usiopungua sentimita 60

  3. Ukiwa na tabia ya kuchezea simu ya mkononi kabla ya kulala na huwezi kuiacha, basi lala chali na kuweka mikono yako juu ya mito au shuka kuliko kuchezea simu katika mazingira ya giza kabisa, bora uwashe taa moja yenye mwanga hafifu, ili mwanga wa simu usichome sana macho yako.

  4. Na ukiwa na tabia ya kuvaa lenzi za kuonea, bora usivae zaidi ya masaa sita kila siku na ukiwa na mafua au ukiongelea bora usivae kamwe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako