• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Namna sahihi ya kula ukiwa unataka kujenga afya

  (GMT+08:00) 2016-06-09 14:34:40

  Watu wanatabia ya kula chakula kingi kabla ya kujenga afya na kunywa kinywaji kitamu baada ya kujenga afya, lakini namna hiyo ya kula siyo nzuri kwa wale wanaotaka kujenga afya na kupata misuli mizuri. Kwa hiyo, bora ufanye hivi:

  Ukitaka kufanya mazoezi aerobiki kama vile kutembea kwa umbali mrefu au kupanda baiskeli, basi kabla ya kufanya hivyo, bora utumie vyakula vyenye mafuta, sukari na protini, kwa mfano unaweza kunywa milkshake iliyotengenezwa kwa karanga, ndizi mbivu n.k. Na bora ule hivyo dakika 60~90 kabla ya kufanya mazoezi ya aina hiyo.

  Na baada ya kufanya mazoezi, baada ya dakika 20~30,bora unywe maziwa yenye chocolate ili kurejesha hali ya mwili wako kuwa ya kawaida.

  Na ukipendelea kufanya mazoezi ya kujenga misuli na kama ukifanya mazoezi hayo na haikufikia saa moja, basi unahitaji kunywa maji kati kati ya mazoezi, lakini ukifanya mazoezi zaidi ya saa moja, basi bora unywe kinywaji chenye vitamin, na baada ya kujenga misuli, basi unahitaji kula chakula chenye protini nyingi ndani ya saa moja

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako