• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Stephen Keshi afariki dunia

    (GMT+08:00) 2016-06-10 08:44:30

    Wakati Dunia inasubiri kumpumzisha Mohammad Ali leo, maumivu mengine yatakayodumu mioyoni mwa wapenzi wa Soka ni kuondokewa na kipenzi chao Stephen Keshi aliyewahi kuwa nahodha wa Timu ya Taifa ya soka ya Nigeria na baadae kocha wa timu ambapo nyakati zote akiwa nahodha mwaka 1994, Super Eagles ilitwaa ubingwa kwa kuilaza Zambia bao 2-1, mjini Tunis na kisha mwaka 2013, mjini Johannesburg Super Eagles kwa mara nyingine ikiwa chini ya ukufunzi wake ikailaza Burkinafaso bao 1-0.

    Rekodi hiyo ilimfanya Keshi kuwa mtu wa pili Barani Afrika kutwaa Ubingwa wa Mataifa Barani Afrika akiwa mchezaji tena nahodha na baadae akiwa kocha. Rekodi kama hiyo ilikuwa inashikiliwa na Mohamed El ghohari wa Misri. Steven Atakumbukwa kwa mchango wake katika soka ya Nigeria ambapo alikuwa kwenye kikosi kilichotinga hatua ya 16 bora mwaka 1994, kwenye fainali za soka kombe la Dunia nchini Marekani pamoja na kusumbuliwa na maumivu ya goti yaliyohitimisha soka yake mapema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako